Papa Francis: Wanaoshambulia Allepo ''watawajibika kwa Mungu''

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis
Image caption Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis

Papa Francis ameshutumu uliapuaji wa mji wa Allepo nchini Syria ,akisema kuwa wale wanaohusika na mauaji watawajibika kwa mungu.

Akizungumza na umati wa watu hadharani katika bustani St. Peters Square mjini Rome,kiongozi huyo wa kanisa katoliki ameutaja mji huo kuwa wa ''mashahidi'' ambapo kila mtu anauawa.

Majeshi ya Serikali ya Syria yanayoungwa mkono na Urusi yameanzisha kampeni kali ya mashambulizi ili kudhibiti maeneo ya mashariki yanayodhibitiwa na waasi.

Mashambulio ya angani yaliendelea usiku kucha kupiga mji huo uliozungukwa.

Papa Francis amezitaka pande zote zinazozozana nchini Syria kuwalinda raia.

''Hili ni jukumu la dharura.Ninawaomba wale wote wanaotekeleza mashambulio katika eneo hilo ,kwamba siku moja watawajibika mbele ya mungu'',alisema.