Iwobi aomba kucheza dhidi ya Wenger katika FIFA

Alexi Iwobi
Image caption Alexi Iwobi

Ifikiapo siku ya Jumamosi Meneja wa Arsenal Arsene Wenger atakuwa ameiongoza klabu hiyo kwa takriban miaka 20.

Hiyo ni miongo miwili katika klabu ambayo jina lake linafanana na herufi nne za kwanza za jina la mkufunzi huyo.

Image caption Iwobi na Wenger

Lakini winga Alexi Iwobi ameambia Newsbeat angependelea kucheza dhidi ya Wenger katika mechi ya mchezo wa video wa FIFA kusherehekea hatua iliopigwa katika klabu hiyo.

''Hajasema lolote kuhusu ni nini kilichopangwa na wachezaji hao ambacho kinaweza kuhusisha ''sherehe na vinywaji''.

Image caption Arsene Wenger alipojiunga na Arsenal na baada ya miaka 20

''Nitashangaa iwapo amewahi kucheza mchezo huo wa FIFA,lakini iwapo hajacheza basi itakuwa matani.Ningependa kucheza dhidi yake,naam''.