Utafiti: Chunusi humfanya mtu kuonekana mdogo

Chunusi huwanfanya vijana kuonekana wadogo kwa muda mrefu
Image caption Chunusi huwanfanya vijana kuonekana wadogo kwa muda mrefu

Iwapo wewe ni kijana ambaye ana chunisi ,unaweza kujihisi kana kwamba ni mwisho wa dunia. Lakini utu uzima wako utakusaidia.

Utafiti mpya kutoka chuo cha Kings mjini London,kilichowachunguza mapacha wa kike 1,205,unasema kuwa kijana aliye na chunusi huishi masha akionekana mdogo ukilinganisha na watu wa umri kama wake ambao wana ngozi nzuri.

Wataalam wanasema kuwa ni kwa sababu watu waliio na acne wana kinga ya mwilini dhidi ya uzee.

Hiyo inamaanisha kwamba vitu kama vile ngozi iliojikunja na ilikonda huonekana baadaye katika maisha.

Kwa nini?

Utafiti huo umechunguza seli nyeupe zilizchokuliwa kutoka kwa mtu mwenye chunusi na kubaini kwamba zina kofia zenye kinga katika mwisho wa kromosomu zake zinazowasaidia kutozeeka haraka.