Majimbo ya Somalia yazozana kutokana na shambulio

Majimbo ya Somalia
Image caption Majimbo ya Somalia

Jimbo la kati la Somalia, Galmudug linasema kuwa zaidi ya wanachama 20 wa kikosi chake cha usalama wameuawa katika shambulio la angani.

Waziri wa usalama wa jimbo hilo Osman Isse alilishtumu jimbo jirani la Puntland kwa kuzua ghasia hizo.

Puntland linasema kuwa wale waliouawa walikuwa wanachama wa kundi la al-Shabab na kwamba sio wanajeshi wa kawaida.

Mamia ya watu katika jimbo la Galmudug wameandamana dhidi ya shambulio hilo.

Walichoma bendera za Marekani na kudai kwamba Marekani ndio iliohusika na shambulio hilo.

Kufikia sasa hakuna tamko lolote kutoka kwa Marekani.

Puntland na Galmudug hukabiliana mara kwa mara kutokana na ardhi na maswala mengine.