Watoto wasioweza kuugua Ukimwi

Virusi vya HIV huua kinga yote ya mwili na kuacha mwili kwenye hatari ya kuambukizwa maradhi mengine. Haki miliki ya picha SPL
Image caption Virusi vya HIV huua kinga yote ya mwili na kuacha mwili kwenye hatari ya kuambukizwa maradhi mengine.

Uchunguzi uliofanywa na wanasayansi wa chuo cha Oxford umeonysha kuwa asilimia 10 ya watoto walioambukizwa virusi vya HIV hawapati ugonjwa wa Ukimwi licha ya kutopata matibabu.

Utafiti uliofanyiwa watoto 170 walio na virusi vya HIV nchini Sudan Kusini ulionyesha kuwa kinga yao ya mwili ililingana na ya nyani waliokuwa na virusi hivyo.

Wataalamu wanasema kuwa ugunduzi huo ni ishara ya kwanza ya watu wanoishi na virusi vya HIV, ambao utasababisha kupatikana na tiba kwa wagonjwa wote walio na virusi hivyo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ikiwa virusi vya HIV haviwezi kutibiwa vinaweza kuwaua asilimia 60 ya watoto katika kipindi cha miaka miwili unusu.

Ikiwa virusi vya HIV haviwezi kutibiwa vinaweza kuwaua asilimia 60 ya watoto walio na virusi hivyo katika kipindi cha miaka miwili unusu.

Kisha virusi hivyo huua kinga yote ya mwili na kuacha mwiwi kwenye hatari ya kuambukizwa maradhi mengine.

Watafiti walichunguza damu kutoka kwa watoto 170 kutoka Sudan Kusini waliokuwa na virusi vya HIV, ambao hawakupata matibabu na ambao hado hawakuwa wameugua ugonjwa wa ukimwi.