India yawashambulia wanamgambo eneo la Kashmir

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Uhusiano kati ya India na Pakistan umedhoofika mieizi ya hivi karibuni

India inasema kuwa imefanya mashambulizi dhidi ya wanamgambo wanaopanga mashambulizi kutoka eneo lilalodhibitiwa na Pakistan la Kashmir.

Jeshi la India halikutoa taarifa zaidi jinsi mashambulizi hayo yalifanyika. Hata hivyo vyombo vya habari nchini India vinasema kuwa makomando walivuka kwa sehemu ndogo upande wa Kashmir nchini Pakistan.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Pakistan inasema kuwa wanajeshi wake wawili waliuawa waakti wa majibizano ya risasi kwenye mpaka

Pakistan imetupilia mbali madai ya mashambulizi hayo ikisema kuwa wanajeshi wawili wa Pakistan waliuawa wakati wa majibizano ya risasi kwennye mpaka yaliyochochewa na India.

Wadadisi wanasema kuwa ikiwa wanajeshi wa India walivuka eneo la mpaka italeta wasi wasi mkubwa kati ya mataifa hayo yenye nguvu ya nuklia.