Yanga na Simba kumenyana Jumamosi

Image caption Yanga katika mechi ya awali

Vigogo ambao pia ni mahasimu wa soka Tanzania bara kutoka mtaa wa kariakoo jijini Dar es salaam, Yanga na Simba,wanatarajia kumenyana katika mechi ya kwanza siku ya Jumamosi October mosi, katika mechi ya ligi kuu ya soka ya Tanzania bara itakayopigwa katika uwanja mkuu wa taifa jijini Dar es salaam.

Mpaka sasa Timu hizo zimejikita kambini kujiandaa kwa mechi hiyo ,Simba mpaka sasa ndio wanaongoza ligi baada ya kucheza Mechi 6 na wana pointi 16 wakifuatiwa na Stand United wenye Pointi 12 kwa Mechi 6. Nafasi ya tatu ni Yanga huku nafasi za nne na tano zipo Azam FC na Mtibwa Sugar zote zikiwa na pointi 10 kila mmoja.

Image caption Klabu ya Simba

Katika kuelekea mechi hiyo makocha wa timu hizo Joseph Omong wa simba na Hans van Pluijim, kila mmoja amesema kuwa timu itaibuka na ushindi.

Msimu uliopita, Yanga iliikung'uta Simba mabao 2-0 katika mechi zote mbili.