Zaidi ya 100 wajeruhiwa kwenye ajali ya treni Marekani

Haki miliki ya picha @BIG_POPPA_CHOP
Image caption Zaidi ya watu 100 wamejeruhiwa na wengine kukwama.

Treni moja imegonga kituo cha reli kwenye mji wa Hoboken ulio jimbo la New Jersey nchini Marekani

Idara inayohusika na huduma za dharura jimba la New Jersey inaripoti kuwa mmoja ameuawa na zaidi ya 100 kujeruhiwa .

Picha kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha uharibifu mkubwa kwa treni na kituo.

Image caption Kituo cha Hoboken kiko umbali ya maili ksaba kutoka mji wa New York

Kituo cha Hoboken kiko umbali ya maili saba kutoka mji wa New York na watu wengi hukitumia kusafiri kwenda mtaa wa Manhattan.

Ben Fairclough ambaye alikuwa eneo hilo aliiambia BBC kuwa treni hiyo ilikuwa imetoka kabisa kwenye njia yake.

"Kulikuwa na watu waliokuwa wameketi chini huku damu ikiwatoka vichwani. Kulikuwa na majeruhi wengi," alisema Fairclough.