Uchumi wa nchi za Afrika washuka hadi asimia 1.6

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Uchumi wa nchi za Afrika ulishuka hadi asilimia 1.6 mwaka 2016

Ukuaji wa uchumia kwenye nchi zilizo kusini mwa jangawa la sahara unatajiwa kushuka hadi asilimia 1.6 mwaka huu kutoka asilimia 3 mwaka 2015.

Hata hivyo ukuaji utakuwa kwa asilimia 2.9 mwaka ujao kwa mujibu wa utafiti wa kila mwaka wa benki ya dunia ambao ulitolewa kwenye mji mkuu wa Ivory Coast Abidjan.

Pia uchumi wa mataiafa ya Afrika unatarajiwa kupanda kwa asilimia 3.6 mwaka 2018.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Uchumi wa mataifa ya nchi kama Tanzania, Ethiopia an Rwanda uliboreka

Huku mataifa mengi ya afrika yakishuhudia kushuka kwa uchumi, baadhi ya nchi zikiwemo Ethiopia, Rwanda na Tanzania zimeendelea kupata ukuaji wa kila mwaka kwa zaidi ya asilimia sita.

Mtaiafa yakiwemo Côte d'Ivoire na Senegal yametajwa kuwa bora zaidi.