ICC kuchunguza ghasia nchini Gabon

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Majengo ya bunge yalitekezwa moto tarehe 31 mwezi Agosti

Mwendesha mashtaka wa mahakama kuu wa kimataifa ya uhalifu wa kivita (ICC) Fatou Bensouda, anasema kuwa anafuatilia ghasia zinazoendelea nchini Gabon kufuatia utata uliokumba uchaguzi wa rais.

Serikali ya Gabon imeomba ICC kufanya uchunguzi ikiwalaumu wafuasi wa kiongozi wa upinzani Jean Ping kwa kuchochea mauaji ya halaiki na uhalifu mwingine dhidi ya binadamu.

Wafuasi wa upinzani walichoma bunge baada ya rais Bongo kutangazwa mshindi kwenye uchaguzi huo wa Agosti 27, huku naye Ping akisema kuwa makao makuu ya chama chake yalipigwa bomu.