Uchaguzi wa Marekani 2016
Habari kuu
Trump ashinda urais Marekani
Donald Trump amemshinda Hillary Clinton katika matokeo ya uchaguzi wa urais uliokuwa na ushindani mkali.
Matokeo ya uchaguzi yatajulikana saa ngapi Marekani?
Maeneo mengi Marekani yalisubiri vituo vifungwe - sana kati ya 19:00 EST (24:00 GMT - Saa tisa usiku Afrika Mashariki) na 20:00 EST (01:00 GMT - Saa kumi usiku Afrika Mashariki) - kuanza kupokea matokeo na makadirio ya matokeo katika majimbo mbalimbali.
Moja kwa moja Obama ampigia simu Trump kumpongeza
Mgombea wa Republican Donald Trump amemshinda Hillary Clinton wa Democratic katika uchaguzi wa urais uliokuwa na ushindani mkali.
Trump alalamika FBI kumuondolea makosa Clinton
Donald Trump amelishambulia shirika la uchunguzi wa jinai nchini Marekani (FBI) kwa kumuondolea makosa minzani wake wa chama cha Demcratic Hillary Clinton.
Uchaguzi Marekani: Nani atashinda?
Uchaguzi mkuu nchini Marekani utafanyika hapo kesho kuchagua atakayemrithi Rais Barack Obama. Je, hali ikoje sasa na nani ana nafasi nzuri ya kushinda?
Bill Clinton ataitwa nani Hillary akishinda?
Hili ni swali ambalo watu wamekuwa wakijiuliza tangu Bi Clinton alipotangaza kwamba angewania urais mwaka jana, na jibu lake si rahisi.
Obama: Mustakabali wa dunia utakuwa kwenye mizani
Rais wa Marekani Barack Obama ametahadharisha kwamba wapiga kura nchini Marekani watakuwa wakiamua kuhusu hatima ya Marekani kama taifa na ulimwengu kwa jumla watakapokuwa wanapiga kura Jumanne.
Obama aonya uchunguzi juu ya barua pepe za Clinton
Rais wa Marekani Barack Obama ameonya kuwa uchunguzi wa shirika la kijasusi la FBI kuhusu barua pepe za Hillary Clinton usiendeshwe kikashfa.
Kila unachohitaji kujua kuhusu uchaguzi Marekani
Tuko katika wiki chache za mwisho za kampeni - haya ndio unayohitaji kuyajua.
Trump: Tuko nyuma lakini hatukati tamaa
Maafisa wa Donald Trump wamekiri kwamba mgombea huyo yupo nyuma ya mpinzani wake Hillary Clinton wa chama cha Democratic zikiwa zimesalia chini ya wiki mbili kabla ya uchaguzi kufanyika.
Clinton atabahatika mara ya pili?
Wasifu wa Hillary Rodham Clinton, mgombea urais wa chama cha Democratic, ambaye ni mama wa taifa wa zamani aliyehudumu pia kama seneta New York na waziri wa mambo ya nje wa Rais Barack Obama kwa miaka minne.
Trump: Nitakubali matokeo ya uchaguzi 'iwapo nitashinda'
Mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amesema kuwa atakubali matokeo ya uchaguzi wa urais nchini Marekani ''iwapo atashinda''
Mtangazaji aliyemhoji Trump afutwa kazi
Shirika la utangazaji la NBC nchini Marekani limemfuta kazi mtangazaji Billy Bush ambaye amekuwa akiendesha kipindi cha Today.
Mke wa Donald Trump ajitokeza kumtetea
Mke wa mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump, Melania, amesema wanawake wanaomtuhumu mumewe kwa kuwadhalilisha kingono ni wanasema uongo, na kusisitiza kwamba Bw Trump ni "mwanamume mstaarabu".
Obama awataka Republican wajitenge na Trump
Rais wa Marekani Barack Obama ametoa wito kwa viongozi wakuu wa chama cha Republican kuondoa rasmi uungaji mkono wao kwa mgombea wa chama hicho Donald Trump.
Pence na Kaine walumbana kuhusu Trump
Mgombea urais mwenza wa chama cha Republican nchini Marekani Mike Pence na mwenzake wa Democratic Tim Kaine wamelumbana kuhusu taarifa za kodi za Donald Trump kwenye mdahalo wa runinga.
Uchaguzi wa Marekani 2016: Yote unayofaa kujua
Mnamo mwezi Januari 2017 ,taifa lenye nguvu zaidi duniani litakuwa na kiongozi mpya baada ya uchaguzi wenye ushindani mkali na gharama kubwa
Trump ''huenda hakulipa ushuru kwa miaka kadhaa''
Gazeti moja nchini Marekani linasema kuwa limepata nyaraka zinazoonyesha kuwa Donald Trump alikuwa ametangaza kupata hasara ya zaidi ya dola milioni 900 mwaka 1995.
Trump apoteza $800m kipindi cha mwaka mmoja
Mfanyabiashara tajiri wa New York anayewania urais kupitia chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amepoteza $800m ya utajiri wake katika kipindi cha mwaka mmoja, kwa mujibu wa jarida la Forbes.
Trump na Clinton walumbana kwenye mdahalo
Wagombea urais nchini Marekani Hillary Clinton na Donald Trump wamepambana vikali katika mdahalo wa kwanza wa televisheni.
Afisi ya Republican yarushiwa bomu Marekani
Lakini Mgombea wa chama cha Republican Donald Trump alionekana akiwalaumu wafuasi wa chama cha Democrat kwa kutekeleza kitendo hicho
Mdahalo kati ya Clinton na Trump, nani aliibuka mshindi?
Lilikuwa ni pambano kati ya wakili na muuza bidhaa, kwa wakati mwingi wakili aliibuka kidedea
Hillary Clinton:Sina tatizo kubwa kiafya
Msemaji wa mgombea kiti cha urais kutoka chama cha Democratic nchini Marekani Bi Hillary Clinton amesema kuwa hana matatizo yoyote ya kiafya zaidi ya uongojwa wa mapafu, na anaendelea na matibabu.
Trump ataka walinzi wa Clinton wapokonywe silaha
Wafuasi wa Bi Hillary Clinton, wamelaani vikali matamshi ya leo ya kejeli aliyotoa Donald Trump, dhidi ya Bi Clinton.
Kenya na Libya zatajwa katika mdahalo Marekani
Kenya na Libya ni miongoni mwa mataifa yaliotajwa wakati wa mdahalo wa urais nchini kati ya Clinton na
Clinton atoa maelezo zaidi kuhusu afya yake
Mgombea wa kiti cha urais wa chama cha Democratic, nchini Marekani, Bi Hillary Clinton, ametoa maelezo zaidi kuhusu jinsi alivyougua ugonjwa wa kichomi.
Obama: Donald Trump ''hana ufahamu''
Rais Barack Obama amemtaja Donald Trump kuwa mtu "wa ajabu" na "asiye na ufahamu" baada ya mgombea huyo wa Republican kusema kuwa rais wa Urusi Vradimir Putin ni kiongozi mzuri zaidi
Trump awaidhinisha mahasimu wake wa Republican
Mgombea wa urais wa chama cha Republican Donald Trump amechukua hatua ya kuboresha uhusiano na uongozi wa chama cha Republican
Mchungaji akatisha hotuba ya Trump Marekani
Mchungaji wa kanisa moja la watu weusi katika jimbo la Michigan, Marekani amemkatisha Donald Trump akihutubu alipoanza kumshutumu mpinzani wake Hillary Clinton.
Trump: Putin anamshinda Obama kwa uongozi
Donald Trump amemlimbikizia sifa rais wa Urusi Vladimir Putin yeye na mpinzani wake Hillary Clinton walipokuwa wakipokea maswali kutoka kwa wanajeshi wastaafu.
Daktari wa Trump asifu afya yake
Daktari wa Donald Trump amesema alitumia dakika tano kuandika waraka wa kuidhinisha afya yake ,huku gari la Bw Trump likimsubiri nje
Wakuu wa Republican wataka chama kikate udhamini kwa Trump
Zaidi ya wakuu wa chama cha Republican 70 wamesaini barua kwa mkuu wa kamati ya kitaifa ya chama hicho wakimtaka aache kusaidia kampeni za Donald Trump.
Video, Waafrika waliohamia Marekani wakati wa Obama, Muda 2,52
Waafrika waliohamia Marekani wakati Rais Obama akiingia madarakani walishuhudia mtikisiko wa kiuchumi. Lakini sasa mambo yameanza kuimarika.
Video, Uhusiano wa Wamarekani Weusi na Waafrika, Muda 2,42
Wakati Marekani ikikaribia kufanya uchaguzi wake, mwandishi wetu Zuhura Yunus anatazama uhusiano wa Wamarekani weusi na wahamiaji kutoka Afrika na jinsi wanavyojiandaa na uchaguzi.
Trump achekwa kwa alivyotamka Tanzania
Mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump amekejeliwa mtandaoni baada ya kuonekana akiboronga akitamka Tanzania wakati wa kutoa hotuba.
Sanders na nduguye watekwa na hisia Philadelphia
Seneta wa Vermont Bernie Sanders na nduguye Larry Sanders watekwa na hisia Philadelphia.
Ndege aingilia mkutano wa Bernie Sanders
Mgombea urais wa chama cha Democratic nchini Marekani Bernie Sanders alikatiza hotuba yake kwa muda baada ya ndege kutua kwenye jukwaa akihutubia mkutano wa kampeni.
Melania Trump ashtaki kuhusu ukahaba
Melania Trump amelishtaki gazeti la Daily Mail la Uingereza pamoja na mwanablogu wa Marekani akitaka alipwe $150m (£114m) kuhusiana na tuhuma kwamba alikuwa kahaba miaka ya 1990.
Trump: Mexico watalipia ukuta '100%'
Mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amesisitiza kwamba Mexico italipia ukuta utakaojengwa mpakani kuzuia raia wake kuingia Marekani asilimia 100 iwapo atashinda urais.
Hillary Clinton augua ugonjwa wa kichomi
Mgombea Urais kutoka chama cha Democratic Hillary Clinton amegundulika kuwa na ugonjwa wa kichomi baada ya kuugua katika tukio la kuwakumbuka wahanga wa shambulio la septemba 11.
Trump azua mjadala tena Marekani
Mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani, Donald Trump, amezua mjadala mpya baada ya kuwahimiza wafuasi wake wenye bunduki kumzuia Clinton.
Wakuu wa Republican wanaomkana Trump
Wakuu wa Republican waendelea kutangaza msimamo wao kuwa hawatampigia kura Bw Trump.
Wataalamu waonya Trump atakuwa 'rais mropokaji'
Wataalamu wa masuala ya usalama nchini Marekani wameonya kuwa Donald Trump atakuwa rais asiye makini zaidi.
Waziri ajiuzulu Mexico kupinga ziara ya Trump
Waziri wa Fedha nchini Mexico, Luice Videgaray amejiuzulu wadhifa wake wiki moja baada ya ziara yenye utata iliyofanywa na mgombea Urais wa Marekani Donald Trump.
Akamatwa kwa kupanda jengo kuu la Trump
Mtu mmoja aliyejaribu kupanda jengo la Trump Tower lililopo jijini New York, ameondolewa na polisi katika jengo hilo baada ya kuchomwa na vioo vya jengo hilo lenye ghorofa 58 ambalo ni makao makuu ya kampeni za kumchagua Donald Trump.
Melania Trump akumbwa na madai kuhusu viza
Mke wa mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amekanusha madai kwamba huenda alivunja sheria za viza alipoanza kufanya kazi nchini Marekani.
Trump alaumu wanahabari kwa utata
Donald Trump amewalaumu waandishi wa habari baada yake kushutumiwa kwa matamshi yake ambapo alidaiwa kuwahimiza wafuasi wake wamuue mpinzani wake Hillary Clinton wa chama cha Democratic.
Trump sasa anaamini Obama alizaliwa Marekani
Afisi ya kampeni ya mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump imetoa taarifa ikisema sasa anaamini Rais Obama alizaliwa nchini Marekani.
Collin Powell: Trump ni ''aibu kwa taifa''
Aliyekuwa waziri wa maswala ya kigeni Collin Powell ameripotiwa kumuita mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama cha Republican Donald Trump ''aibu kwa taifa''
Trump akereka mshukiwa wa New York kutibiwa
Mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amelalamikia hali kwamba mshukiwa anayedaiwa kutekeleza shambulio New York Ahmad Khan Rahami alitibiwa baada ya ufyatulianaji risasi na maafisa wa polisi.
Trump: Tajiri anayetaka kuingia White House
Donald Trump ni tajiri anayemiliki majumba mengi na huwa anajizatiti sana kushinda; anasema ni lazima afanikiwe kuwa Rais wa Marekani.
Msema kweli: Mdahalo wa Clinton na Trump
Huu hapa ni muhtasari wa ukweli kuhusu baadhi ya masuala yaliyoibuka wakati wa mdahalo wa kwanza kwenye televisheni baina ya Hillary Clinton na Donald Trump.
Mkusanyiko wa picha, Kwa Picha: Vinyago vya utupu vya Trump
Huu hapa ni mkusanyiko wa picha kutoka Marekani, ambapo vinyago vya utupu vya mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump viliwavutia sana wapita njia.