Vyoo vilivyojengwa kwa vioo vyazinduliwa nchini China

Mwanamume chooni Changsha, China, 29 Septemba 2016. Haki miliki ya picha Barcroft
Image caption Vyoo hivyo vimezingirwa na msitu

China imezidisha matumizi yake ya vioo kuunda vivutio vya kitalii kwa kujenga choo cha vioo ambacho mtu anaweza akaona nje na hata ndani.

Vyoo hivyo, vimejengwa karibu na Ziwa Shiyan, katika mkoa wa Hunan kusini mwa nchi hiyo.

Vioo hivyo vinawezesha wanaovitumia vyoo hivyo kutazama mandhari ya kuvutia ya msitu au wengine wanaotumia vyoo jirani.

Aidha, walio nje wanaweza kuona walio ndani ya vyoo.

Kuta za vyoo hivyo, hata zile zinazotenganisha vyoo vya wanawake na wanaume, ni za vioo kabisa ingawa vioo hivyo vimetiwa ukungu kiasi.

Vyombo vya habari nchini humo vinasema ni watu wachache sana waliotumia vyoo hivyo siku ya kuzinduliwa kwake.

Haki miliki ya picha Barcroft Images
Image caption Wenye haya wanaotaka kwenda haja ndogo wanaweza kutulizwa na hali kwamba kuna eneo lisilo la vioo la kujikinga

Licha ya umaarufu wa mijengo ya kutumia vioo katika ujenzi, hasa kwenye madaraja na barabara, baadhi ya miradi imefungwa.

Haki miliki ya picha Barcroft
Image caption Mfanyakazi akifanya usafi kwenye vyoo hivyo
Haki miliki ya picha Barcroft
Image caption Kuta za kutenganisha vyoo, hata vile vya wanaume na wanawake, vimetiwa tu ukungu kidogo

Habari za kuzinduliwa kwa vyoo hivyo zimevuma sana.

Ejike Nnadi, akichangia ujumbe wa Facebook wa runinga ya taifa CCTV amesema: "Hapana".

Lakini kunao wengine wanaosema wanaweza kujaribu kuvitumia.

Haki miliki ya picha Barcroft
Image caption Vyoo hivyo vinapatikana eneo la milimani

Tina Chen anasema mradi huo wa vyoo ni ishara kwamba kuna mtu alikuwa na pesa za "kupoteza".

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kuna njia ya vioo iliyojengwa juu mlimani Tianmen

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii