Winnie Mandela aibiwa dola 6000 kutoka nyumbani kwake

Winnie anasema alipewa pesa hizo wakati wa sherehe ya siku yake ya kuzaliwa alipohitimu miaka 80

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Winnie anasema alipewa pesa hizo wakati wa sherehe ya siku yake ya kuzaliwa alipohitimu miaka 80

Polisi nchini Afrika kusini wanasema wanachunguza kesi ambapo aliyekuwa mke wa rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela, Winnie Madikizela Mandela aliibiwa pesa kutoka nyumbani kwake.

Msemaji wa polisi anasema kuwa hawajamkamata mshukiwa yeyote lakini wanaendelea na uchunguzi.

Mtandao wa News24 ulisema kuwa Winnie Mandela aligundua kuwa dola 6,000 ambazo alikuwa amepewa kama zawadi wakati ya sherehe ya siku ya kuzaliwa kwake zilikuwa zimetoweka

Mtandao huo unasema aligundua kuwa hazikuwepo wakati alienda kutafuta pesa kumtuma mtu anunue mkate.

Ripoti zinasema kuwa alikuwa na mipango ya kuzipeleka pesa hizo kwenye benki.