Wenger: Wachezaji wa Afrika wamenifaa sana katika soka

Arsene Wenger ameongoza Arsenal kwa miaka 20 Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Arsene Wenger ameongoza Arsenal kwa miaka 20

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ameiambia BBC kuwa wachezaji kutoka nchi za Afrika wamekuwa wenye umuhimu mkubwa katika taaluma yake ya miaka 20.

Wenga alikuwa akizungumza wakati wa mkutano wake wa kawaida na waandishi wa habari kabla ya mechi ambapo pia alitunukiwa kwa kukiongoza klabu hicho kwa miongo mwili.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Nwankwo Kanu wa Nigeria alikuwa mmoja wa wachezaji waliokuwa wenye umuhimu mkubwa kwa Arsene

Akiwa mwenye uso uliotabasamu, Wenger amesena kuwa wachezaji kutoa Afrika wana moyo, wenye ubunifu na nguvu, masuala ambayo ni vigumu kuyapa kwenye mchezo.

Aliwataja wachezaji akiwemo Nwanko Kanu wa Nigeria, Kolo Toure wa Ivory Coast na gwiji raia wa Liberia George Weah, ambaye alikuwa meneja wake katika klabu ya Monaco nchini Ufaransa, kama wachezaji watatu waliokuwa na uswawishi mkubwa katika taaluma yake.

Image caption Wenger akihutubia wanahabari Ijumaa