Maisha ya wachuuzi barani Afrika

Inaaaminika kuwa zaidi ya nusu la pato la taifa barani Afrika hutokana na sekta ndogo ndogo ambazo huchukua asilimia 80 ya ajira zote, huku sehemu kubwa wakiwa ni wafanyibiashara wadogo wadogo. Sasa swali ni je serikali zinaweza kudhibiti wafanyibiashara? wachuuzi hawa wanaiambia BBC kuhusu maisha yao.

Haki miliki ya picha BBC's Boldwill Hungwe
Image caption Beauty Nyandoro mwenye umri wa miaka 26 anauza mboga na matunda mjini Harare Zimbabwe. Anasema ushindani ni mkubwa kwa sababu anauza karibu na duka la jumla. Anasema kipato chake ni karibu dola 100 kwa mwezi ambazo huzitumia kukidhi mahitaji ya familia yake ua watu watatu.
Haki miliki ya picha BBC's Randy Joe Saah
Image caption Peter Nkemashi kutoka Cameroon alikuwa na ndoto ya kuwa hakimu. Kwa sasa anamiliki duka mjini Yaounde. anasema ana cha kumtosha na familia yake. Hiyo ndiyo ninaita kuwa maisha mazuri.
Haki miliki ya picha BBC's Lucy Walker
Image caption Lakini katika nchi nyingi za Afrika wachuuzi hujipata kwenye malumbano na utawala ulio na naia ya kuwaondoa barabarani .
Haki miliki ya picha BBC's Patience Atuhaire
Image caption Sandra Birabwa, mwenye umri wa miaka 24, anasema watu humuita "Sandra Leggings" kutokana na muda anaotumia kuzunguka mitaa ya mji wa Kampala akiuza nguo. Anasema ana matumaini ya kufungua duka lake lakini kwa sasa kodi ni ya juu sana.
Haki miliki ya picha BBC's Rana Jawad
Image caption Mohamed El-Hed, mwenye umri wa miaka 63, anaishi mjini Tunis nchini Tunisia akiuza michoro na kukimu familia ya watu watano. Anasema amekuwa akifanya kazi hiyo kwa miaka 16 tangu astaafu kutoka kazi yake la kiwandani.i Ninataka watoto wangu wapate kazi zinazowafaa.
Haki miliki ya picha BBC's Alhassan Sillah
Image caption Mamadou Saliou Barry anauza sells CDs and DVDs mjini Conakry, Guinea. Mambo ni magumu kwa sababu wanamuziki wengi wanatulaumu kwa kunakili CD zao. Kwa hivyo wao hutuhangaisha sana.
Haki miliki ya picha BBC's Umaru Fofana
Image caption Comfort Conteh kutoka nchini Sierra Leonean anapata faida ya dola 8 kwa kuuza mikate kwenye mji mkuu Free Town na huwakidhi mamake na mtoto. Anasema alisomea taaluma ya kuoka mikate lakini hakuikamilisha. Anasena angependa kurudi kusoma ili pate kazi nzuri.
Haki miliki ya picha BBC's Sammy Awami
Image caption Mohammed, mwenye umri wa miaka 28, anauza bidhaa za simu mjini Dar es Salaam Tanzania . Analipia wadogo wake karo na anasema ameifanya kazi hiyo kwa muda mrefu na hataki kufanya kitu kingine tena. Anasema angependa kuona ikipanuka.
Haki miliki ya picha BBC's Jonathan Paye-Layleh
Image caption Moses Tamba naye anauza bidhaa za simu mjini Monrovia Liberia. Anafanya hivyo kujilipia karo. Anasema alipoteza bidhaa za gharama ya dola 300 kwa siku moja wakati utawala ulipomkonya bidhaa zake.