Samsung kuuza tena Galaxy Note 7

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Takriban simu, Galaxy Note 7, milioni mbili laki tano zilirejeshwa kutoka maeneo mbalimbali ulimwenguni, ili kupata btari mpya.

Samsung imeanza mauzo ya simu yake, Galaxy Note-Seven nchini korea kusini, baada ya kusitisha mauzo yake mwezi mmoja uliopita, kutokana na madai kwamba simu hizo zinalipuka.

Kampuni hiyo inasema hitilafu kwenye batri zake zilisababisha milipuko hiyo.

Takriban simu milioni mbili laki tano zilirejeshwa kutoka maeneo mbalimbali ulimwenguni, ili kupata btari mpya.

Makampuni ya usafiri wa ndege yamekuwa yakiwaonya wateja wake dhidi ya kutumia simu hiyo ndani ya ndege.

Hata hivyo sio simu zote zilizo na hitilafu kwenye batri zilizorejeshwa, na hivyo haijulikani wazi wakati marufuku ya kutumia simu hizo ndani ya ndege itakapoondolewa.

Samsung inatoa simu za bure kwa wale walioathirika huku wafanyibiashara wa simu hizo wakipata mali mpya huku simu zaidi zikiendelea kufikishwa sokoni

''Tumetoa wito kwa waathiriwa wa simu hizo kuzibadilisha haraka iwezekanavyo. Simu ya galaxy Note 7 zenye betri ishara ya betri ya kijani zilikuwa salama kutumia'',Samsung imesema.

Image caption Simu aina ya Samsung Galaxy Note 7 iliolipuka