Mji wa Aleppo washambuliwa tena

Hospitali hiyo pia ilishambuliwa mapema wiki jana. Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Hospitali hiyo pia ilishambuliwa mapema wiki jana.

Mashambulizi ya angani yanayoendelea katika mji unaoshikiliwa na waasi wa Allepo nchini Syria, yamegonga hospitali.

Kundi la Syrian American Medical Society, linalofadhili hospitali hiyo linasema kwamba hospitali hiyo ilishambuliwa kwa makombora mawili.

Hospitali hiyo pia ilishambuliwa mapema wiki jana.

Ripoti zinaibuka kwamba vikosi vinavyoungwa mkono na Urusi pamoja na vikosi vya Syria vinashambulia mji wa kale wa Allepo, na kukabiliana na waasi katika mitaa mbalimbali.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mji wa Aleppo umekumbwa na uharibifu mkubwa