Waumini wasusia misa ya papa Georgia

Papa Francis

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Papa Francis

Papa Francis ambaye anafanya ziara yake nchini Georgia ameongoza ibada ya misa ambayo ilihudhuriwa na watu wachache mno, baada ya viongozi wa kanisa la Orthodox kuwataka waumini wao kutoshiriki katika ibada ya wakatoliki.

Ujumbe kutoka kanisa hilo la Orthodox ulitarajiwa kuhudhuria ibada hiyo, japo hawakuhudhuria.

Wakati papa francis aliwasili nchini Georgia alilakiwa na waandamanaji wachache wa kanisa la Orthodox, waliokuwa wakiituhumu Vatican kuwa mnyanyasaji wa kidini.