Rais wa Korea Kusini atoa wito kwa watu nchini Korea Kaskazini kuhamia Kusini

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rais Park Geun-hye ametoa wito kwa watu nchini Korea Kaskazini wakimbie kwenda Kusini

Rais wa Korea Kusini, Park Geun-hye, ametoa wito kwa watu nchini Korea Kaskazini, waikimbie nchi yao, na wzende Korea Kusini.

Katika hotuba yake, alisema anajua dhiki kubwa za maisha nchini Korea kaskazini.

Aliwaambia watu wa Korea Kaskazini kuwa wanaweza kuanza maisha mapya katika nchi huru, ya Korea Kusini.

Image caption Zaidi ya watu 30,000 wamekimbia Korea Kaskazini miaka ya nyuma

Katika miaka iliyopita, watu 30,000 wamejitia katika hatari kubwa na kuikimbia nchi yao.

Juzi, mwanajeshi wa Korea Kaskazini, alikimbilia kusini, kwa kuvuka mpaka baina ya nchi mbili hizo ambao ni wenye ulinzi mkali.