Kimbunga kikali chaelekea Jamaica

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Watu wamesomba bidhaa zote kwenye supermarket, ili kuwa na akiba nyumbani.

Kimbunga kikali kabisa kutokea katika mwongo mzima, kinavuma eneo la bahari kando ya Caribbean, na nchi kama Jamaica, Haiti na Cuba ziko hatarini.

Wakati mmoja Kimbunga Matthew, kilifika nguvu ya kiwango cha 5 -kiwango kikubwa kabisa katika vipimo vya vimbunga,kikiwa na kasi ya kilomita 250 kwa saa.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bidhaa kama maji vinahitajika kwa wingi nchini Jamaica

Lakini sasa kimepungua kasi kidogo, lakini watabiri wa hali ya hewa, wanasema kinaweza kusababisha uharibifu mkubwa.

Bunge la Jamaica limeitisha kikao cha dharura, kujadili matayarisho kwa kimbunga hicho.

Inaripotiwa watu wame-somba bidhaa zote kwenye supermarket, ili kuwa na akiba nyumbani.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii

Kuhusu BBC