Trump ''huenda hakulipa ushuru kwa miaka kadhaa''

Donald Trump huenda hakulipa ushuru kwa miaka kadhaa kutokana na hasara kubwa ya kibiashara aliyopata kulingana na New York Times
Image caption Donald Trump huenda hakulipa ushuru kwa miaka kadhaa kutokana na hasara kubwa ya kibiashara aliyopata kulingana na New York Times

Gazeti moja nchini Marekani linasema kuwa limepata nyaraka zinazoonyesha kuwa Donald Trump alikuwa ametangaza kupata hasara ya zaidi ya dola milioni 900 mwaka 1995.

Gazeti la The New York Times linasema kwa hasara hiyo ilikuwa kubwa zaidi na ingemwezesha mgombea huyo wa urais wa chama cha Republican kutolipa ushuru kwa zaidi ya miaka 18 kisheria.

Kampeni ya bwana Trump ambayo imekataa kutoa rekodi zake za ushuru na haikukubali wala kukana hasara ambazo Trump amepata.

Katika taarifa imesema kuwa Trump ni mfanyibiashara hodari ambaye alijua sheria kuhusu ulipaji ushuru zaidi ya mtu yeyote yule ambaye amewahi kgombea urais.