Colombia kuamua kuhusu makubaliano ya amani

Makubaliano ya amani nchini Colombia kati ya waasi na serikali
Image caption Makubaliano ya amani nchini Colombia kati ya waasi na serikali

Watu nchini Colombia wanapiga kura ya maoni kuamua ikiwa watakataa au kukubali makubaliano ya amani kati ya serikali na waasi wa FARC.

Makubaliano hayo yalitiwa sahihi siku ya Jumatatu na rais Juan Manuel Santos pamoja na kiongozi wa waasi wa FARC kwa jina Timochewnko ambaye aliwamba msamaha waathiriwa wa mzozo huo ambao ulidumu kwa miaka 52.

Chini ya makubaliano hayo FARC watasalimisha silaha zao na kumaliza kuhusika kwake katika biashara ya madawa ya kulevya na kukubalika na kuwa chama cha kisiasa, huku wahusika wa uhalifu wa pande zote mbili wakifikishwa mbele ya sheria.

Mzozo huo umesababisha vifo vya watu 200,000 na kuwalazimu wengine milioni 6 kuhama makwao.

Tayari waasi wa FARC wamesema kuwa watawalipa fidia waathiriwa wa mgogoro huo wa miaka 52 wakati huu ambapo taifa hilo linapiga kura ya maamuzi .