Rwanda kudhibiti mwendo kasi,kupunguza ajali barabarani

Image caption Magari ya abiria nchini Rwanda

Wamiliki wa magari ya abiria na uchukuzi wa mizigo nchini Rwanda,wameagizwa kuweka mashine zinazodhibiti mwendo wa kasi (Speed governor) katika magari yao ili kupunguza ajali za barabarani.

Image caption Mashine ya kupunguza mwendo kasi

Jean Pierre Rukundo kutoka kampuni ya BENO Cars Limited ambayo imepewa la jukumu la kuweka mashine hizo za kupunguza kasi,anasema "Mwendo wa gari unapofika kwa kasi ya Km 55 kwa saa,gari linaanza kutoa tahadhari na unapong'ang'ana labda kuzidisha kasi ya km 60 kwa saa,unarudishwa chini kwenye kasi iliyo kati ya km 25-30 kwa saa moja"

Huku baadhi ya waendesha magari wanasema hawana wasi wasi wowote juu ya uamzi huo ingawa wengine wanaona kwamba mashine hizi zitawapunguzia kipato walichokuwa wanaingiza kwa kufanya safari nyingi kwa siku.

Image caption Moja ya kituo cha daladala nchini Rwanda

Hatua hii itajumuisha magari zaidi ya elfu 6000 yanayofanya kazi ya uchukuzi wa abiria na mengine yanayosafirisha mizigo,huku magari ya watu binafsi yakiwa bado hayajahusishwa katika mpango huu.Aidha Hakuna lolote lililotangazwa kuhusu usafiri wa pikipiki ambao pia husababisha ajali nyingi barabarani.