Benki ya dunia;Umaskini wapungua Asia

Haki miliki ya picha Google
Image caption Moja ya mtaa,nchini Indonesia

Kiwango cha umaskini uliokithiri duniani kinaendelea kupungua pamoja na kwamba uchumi unaongezeka kwa kiwango kidogo.

Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, idadi ya watu ambao walitajwa kuwa ni maskini kupita kiasi mnamo mwaka 2013 walikuwa milioni mia nane, ambapo mwaka uliofuata idadi hiyo ilipungua kwa milioni moja.

Imeelezwa kwamba, hiyo ni kutokana na maboresho yaliyofanyika ya hali ya maisha katika bara la Asia hasa China, Indonesia na India.

Pamoja na mabiliko hayo, Benki ya Dunia imetaka jitihada zaidi zichukuliwe ili kukabiliana na usawa wa mali ili kufikia lengo la kutokomeza umaskini ifikapo mwaka 2030.