UN: Miji Afrika haijajiandaa vilivyo
Huwezi kusikiliza tena

UN: Miji Afrika haijajiandaa kushughulikia ongezeko la watu

Leo ni siku ya kimataifa ya makazi Duniani na ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa kuhusu miji duniani inabashiri kuwa idadi ya watu wanaoishi mijini barani Afrika itaongezeka mara dufu ifikapo mwaka wa 2030.

Miji barani Afrika inapanuka kwa kasi ya juu zaidi, karibu mara 11 ya kasi ya ukuaji wa miji ya bara Ulaya.

Hata hivyo Afrika haijajiandaa vya kutosha kukabiliana na madhara ya kupanuka kwa miji na kuongezeka kwa idadi ya watu, hivyo kuhatarisha maisha wengi hususan wanaoishi katika vitongoji duni.

Mwandishi wa BBC Anthony Irungu alitembelea mtaa wa Huruma, Nairobi na kuandaa taarifa hii.