Waziri wa Kenya ''kuwania uenyekiti wa tume ya AU''

Waziri wa maswala ya kigeni nchini Kenya kuwania wadhfa wa mwenyekiti wa umoja wa Afrika AU
Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Kenya kuwania wadhfa wa mwenyekiti wa umoja wa Afrika AU

Kenya imewasilisha jina la waziri wake wa maswala ya kigeni Amina Mohamed kuwania wadhfa wa uenyekiti wa tume ya umoja wa Afrika AU.

Mwenyekiti wa sasa Nkosazana Dlamini Zuma ambaye alitarajiwa kujiuzulu mnamo mwezi Julai wakati wa kikao cha umoja huo mjini Kigali Rwanda,aliamua kusalia uongozini hadi kikao chengine baada ya wagombea watatu waliokuwa wakigombea wadhfa huo kushindwa kupata thuluthi mbili za wingi wa kura.

Image caption Habari hiyo ilichapishwa katika mtandao wa Twitter na gazeti la Daily Nation nchini Kenya