Trump ashutumiwa kwa 'kuwabagua wanawake'

Donald Trump
Image caption Donald Trump

Mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama cha Republican Donald Trump ameshtumiwa na wagombea pamoja na wafanyikazi wa kipindi cha The Apprentice of Sexism ,kulingana na uchunguzi wa AP.

Zaidi ya watu 20 waliohojiwa walielezea tabia za bwana Trump kwa wanawake kuwa mbaya na zisozokubalika.

Hatahivyo kampeni ya mgombea huyo imekana madai hayo.

Msemaji wake Hope Hicks alisema kuwa madai hayo ''sio ya kawaida,hayana msingi na ni ya uongo''.

Bwana Trump amekabiliwa na madai kadhaa katika kipindi cha wiki moja iliopita yaliohoji hali yake ya kiafya kuwa rais wa Marekani.

Siku ya Jumapili,gazeti la New York Times lilichapisha ushahidi uliodai kwamba bwana Trump huenda hakulipa ushuru kwa miaka 20.

Wagombea wa zamani pamoja na wafanyikazi wa kipindi cha The Aprentice walielezea vile Trump mara kwa mara alizungumzia ukubwa wa matiti ya wanawake na nani angependa kushiriki naye ngono.

Aliyekuwa mtengezaji wa kipindi hicho Kathrine Walker alisema kuwa Trump mara kwa mara alizungumza kuhusu miili ya wanawake na kusema ni mgombea yupi wa kike anadhani angekuwa mzuri kitandani.