Maandamano mapya ya kupinga serikali yazuka Ethiopia

Waandamanaji wakikabiliana na maafisa wa polisi nchini Ethiopia
Image caption Waandamanaji wakikabiliana na maafisa wa polisi nchini Ethiopia

Maandamano mapya ya kupinga serikali ya Ethiopia yamefanyika, siku moja tu baada ya watu kadhaa kufariki kutokana na mkanyagano, baada ya ghasia kutokea katika mkutano mmoja wa kitamaduni.

Walioshuhudia wanasema kwamba, polisi wamewarushia vitoa machozi waandamanaji katika miji katika maeneo ya kabila la Oromo.

Serikali inasema kuwa watu 55 walifariki katika maandamano ya hapo jana Jumapili, huku upinzani ukipinga na kusema kuwa idadi ya maafa ni kubwa.

Watu wa jamii ya Oromo na Amhara, makabila makubwa mawili nchini Ethiopia wamekuwa wakiandamana kupinga kile wanachosema ni kutengwa kiuchumi na kisiasa.