Taa zatumiwa kuunda vipokea mawimbi vya runinga Sierra Leone

Taa zatumiwa kuunda vipokea mawimbi vya runinga Sierra Leone

Mjini Freetown, Sierra Leone, vijana wamekuwa wakiunda vipokea mawimbi kwa kutumia taa za umeme.

Alhaji Sheku Turay, 29, ni mmoja wa wajasiriamali wanaoviunda na anasema alijifunza kuviunda miaka miwili iliyopita.

Kupitia mradi huo, vijana huwa wanapata faida nzuri na kuwapa kitu cha kujishughulisha nacho.

Hilo huwazuia kujihusisha na uhalifu.