Mzozo wa Syria: Marekani yasitisha mazungumzo na Urusi

Madhara ya vita Syria Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Madhara ya vita Syria

Marekani imetangaza kusimamisha mazungumzo na Urusi kuhusu Syria.

Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marekani imesema Moscow haijafuata masharti ya makubaliano yaliyofikiwa mwezi uliopita ya kusitisha mapigano.

Imesema pia Urusi imeshindwa kuhakikishia serikali ya Syria kubaki katika makubaliano, na kuzilaumu nchi zote kuongeza mashambulizi dhidi ya raia kwa kulenga hospitali na misaada ya kibinadamu inayotolewa.

Hata hivyo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi imesema imesikitishwa na uamuzi huo.

Msemaji wa wizara hiyo ameilaumu Marekani kwa kujaribu kuhamishia lawama kwa Urusi baada ya kushindwa kukidhi masharti ya makubaliano hayo yenyewe.