Trump ajigamba kuhusu ulipaji kodi nchini Marekani

Donald Trump,mgombea urais kupitia chama cha Republican
Image caption Donald Trump,mgombea urais kupitia chama cha Republican

Mgombea wa kiti cha urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump, ambaye amekuwa akishinikizwa kuchapisha malipo yake ya kodi, amejigamba akisema ametumia sheria ipasavyo kulipa ushuru wa chini zaidi kuambatana na sheria.

Amewaambia wafuasi wake kuwa ni jukumu lake kama mfanyabiashara kutumia sheria za kodi kujinufaisha na wawekezaji na wafanyakazi wake.

Donald Trump aliwaambia hayo wafuasi wake wakati akiwa katika jimbo la Pueblo lililopo Colorado na kudai kuwa lilikuwa jukumu lake yeye kama mfanyabiashara kutumia vipengele vya sheria za kodi ili aweze kunufaika nazo yeye mwenyewe, wawekezaji na wafanyakazi wake.

Hivyo amesema anachukizwa sana jinsi anavyoona jinsi Marekani inavyotumia kodi.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Hillary Clinton kutoka chama cha Democratic

Kwa upande wake, mpinzani wake kutoka chama cha Democratic, Hillary Clinton aliwaambia wafuasi wake wakati akihutubia mkutano wa hadhara huko Akron, Ohio kwamba Trump anataka kutumia vibaya baadhi ya vipengele vya sheria za kodi na kuongeza kuwa Trump aliwahi kuwaangusha au kutowasaidia wafanyabiashara wadogo pamoja na kuwaacha njia panda wafanyakazi wake.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii