Colombia kujadili muafaka wa amani

Image caption Rais wa Colombia, Juan Manuel Santos

Rais wa Colombia, Juan Manuel Santos amekutana na kiongozi wa upinzani ili kujadili jinsi ya kupata njia mbadala ya kurejesha amani katika taifa hilo.

Mkutano huu unafanyika mara tu baada ya wapiga kura kupinga makubaliano ya amani yaliyofikiwa kati ya serikali na waasi wa FARC.

Rais huyo aliteua afisa mkuu kutoka serikalini ili kujali njia ambazo zitaweza kuwasaidia kurejesha historia ya makubaliano ya amani na kundi la FARC ambalo limekuwa katika mapambano ndani ya taifa hilo katika kipindi cha nusu karne.

Rais wa zamani Alvaro Uribe wa nchi hiyo, ambaye aliongoza kampeni ya kukataa makubaliano hayo hakuudhuria mkutano huo na kuunda timu yake mwenyewe.

Rais huyo wa zamani anataka waasi waliofanya uhalifu kuchukuliwa hatua kwa kuwekwa gerezani na baadhi ya viongozi wa FARC kufungiwa kujihusisha na kisiasa.

Nae kiongozi wa FARC, Timochenko, anasema ataendelea kuheshimu makubaliano yaliyofikiwa.