Kiongozi wa Muslim Brotherhood auawa Misri

Wizara inasema Kamal alililisimamia tawi lililojihami la Muslim Brotherhood Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wizara inasema Kamal alililisimamia tawi lililojihami la Muslim Brotherhood

Kiongozi wa juu wa kundi la Muslim Brotherhood ameuawa na vikosi vya wizara ya mambo ya ndani Misri, wizara hiyo inasema.

Katika taarifa yake, wizara hiyo imesema Mohamed Kamal ameuawa katika mapmbano ya bunduki na mfuasi mwingine wa kundi hilo Jumatatu.

Wizara imesema Kamal alilisimamia tawi lililojihami la kundi hilo, licha ya kuwa Muslim Brotherhood linasisitiza kuwa ni kundi la amani.

Alihukumiwa kifungo cha maisha gerezani baada ya kushtakiwa kwa makosa mawili pasi kuwepo mahakamani .

Muslim Brotherhood limesema alitoweka siku ya Jumatatu.