Toyota imezindua roboti 'mtoto'

Haki miliki ya picha Toyota

Roboti inayotosha katika kiganja cha mkono inayoweza kuzungumza itauzwa Japan mwaka ujao, kampuni ya Toyota imetangaza.

Kirobo Mini, imeundwa kwa urefu wa 10cm kwa lengo la kuwa na kumzungumzia mmiliki wake, kampuni hiyo imesema.

Inaweza kufanya mazungumzo kujumuisha kauli kuhusu safari, kutokana na data ya gari la mmiliki wake.

Imeundwa pia mithili ya mtoto, lakini mtaalamu wa roboti ameimbia BBC kwamba katu roboti hawezi kuchukuwa nafasi ya mtoto.

"Hucheza kidogo, na hii ni katika kumuigiza mtoto aliyekaa, ambaye hajajua kukaa vizuri," Fuminori Kataoka, mhandisi mkuu wa Kirobo Mini ameliambia shirika la habari la Reuters.

"udhaifu huu umenuiwa kuzusha hisia kwa mmilika wake."

Haki miliki ya picha Getty Images

Prof Dr Kerstin Dautenhahn, kutoka taasisi ya sayansi ya kompyuta kutoka chuo kikuu cha Hertfordshire, amesema roboti hio huenda ikwavutia vijana.

"Inanikumbusha Tamagotchi - fikra ya kuwa ni kitu kidogo kizuri ambacho hakikupi fikra kuwa kiko hai lakini ni tabia tu kama za mtu hai," ameiambia BBC.

Hatahivyo , Prof Dautenhahn, amesema ni vibaya kuamini kuwa kinaweza kuchukuwa nafasi ya mtoto kwa wanawake wasi na watotokama baadhi ya ripoti zinavyoashiria.

'Mazungumzo ya kawaida'

Toyota inasema Kirobo Mini inaweza:

  • Kuzungumza kutumia ishara, kubadili sura na kupesa macho
  • Kukumbuka matukio yaliopita, kama anachopenda mtu, asichopenda
  • Kutumia data kutoka vifaa vilivyopo ndani ya nyumba au gari ili kufanikisha mazungumzo

Huenda ikauzwa kwa takriban £300, na hakuna mipango ya kuiuza nje ya Japan.

Roboti iliotangulia Kirobo Mini yenye urefu wa 34cm iliitwa Kirobo, na ilitumwa katika kituo cha kimaifa cha anga za juu 2013.

Ilinuiwa kufuatana na mwana anga ya juu kutoka Japan Kochi Wakata kama sehemu ya utafiti kuhusu kujitenga