Kabila: Hali ni shwari DR Congo
Huwezi kusikiliza tena

Rais Kabila: Hali ni shwari DR Congo

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila amepuuzilia mbali madai kwamba kuna mvutano wa kisiasa nchini mwake.

Badala yake amevinyooshea kidole vyombo vya habari akisema vinapotosha halisi iliyopo nchini humo.

Mwishoni mwa wiki tume ya uchaguzi ya nchini humo ilitangaza kusogeza mbele tarehe ya uchaguzi hadi mwaka 2018, jambo linalopingwa na upinzani kuwa ni njama za kumuongezea muda wa utawala Rais Kabila.

Tayari zaidi ya watu 50 wameripotiwa kuuawa na Polisi kutokana na maandamano ya upinzani hivi karibuni waliokuwa wakimpinga rais huyo.

Rais Kabila alikuwa akiongea leo wakati wa ziara yake nchini Tanzania.