Vijana wakwamisha Uchaguzi DRC

Image caption Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo akiwa Tanzania

Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo Joseph Kabila ametupilia mbali shutuma kwamba amesogeza mbele tarehe ya uchaguzi ili aendelee kung'ang'ania madarakani.

Rais Kabilla amewaambia waandishi wa habari jijini,Dar es salaam kuwa lengo kuu la Serikali yake kubadili ratiba ya uchaguzi ni kutokuwa na maandalizi ya kutosha.

Amesema serikali yake isingependa kuacha idadi kubwa ya wananchi wake na wengi wao wakiwa ni vijana ambao hawakujiandikisha kupiga kura na wakose haki yao ya kupiga kura .

Mwishoni mwa wiki iliyopita,kiongozi wa tume ya uchaguzi nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo alitangaza uwezekano wa kusogezwa tarehe ya kupiga kura hadi hapo desemba 2018.

Image caption Moja ya maandamano Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo

Siku za hivi karibuni Jamuhuri ya demokrasia ya Kongo imekuwa ikikumbwa na maandamano ya mara kwa mara ambayo yamekuwa yakilenga ucheleweshwaji wa uchaguzi nchini humo.