Haiti yakumbwa na kimbunga kikali

Kimbunga cha Matthew
Image caption Kimbunga cha Matthew

Kimbunga Matthew kimeharibu miundombinu muhimu kama vile barabara ambapo maafisa wanasema kuanguka kwa daraja kumegawa sehemu ya kusini na sehemu nyengine ya nchi.

Image caption Eneo lililopigwa na kimbunga Haiti

Mtu mmoja mpaka sasa amepoteza maisha nchini Haiti na wengine wanne kutoka nchi jirani ya Jamuhuri ya Dominica.

Bado mpaka sasa haijafahamika kiwango cha uharibifu wa kimbunga hicho nchini Haiti, lakini nyumba nyingi zimebomolewa, huku barabara zikiwa hazipitiki kutokana na miti iliyoanguka pamoja na mafuriko.

Image caption Maji yakitiririka Port-au-Prince

Wahanga wa kimbunga hicho wanaendelea kujaa katika makazi yaliyotengwa na serikali katika mji mkuu wa Port-au-Prince huku mamlaka ikiendelea kuomba msaada wa maji pamoja na chakula.