Jeni za watu zavutiwa na 'ladha ya chakula chenye mafuta'

Mchuzi wa Kuku wa mafuta Haki miliki ya picha Thinkstock
Image caption Baadhi ya watu wa jeni zinazovutiwa na chakula cha mafuta

Utafiti mpya unasema baadhi ya jeni za watu zinawafanya kupenda kula chakula kitamu na kilicho na mafuta mengi, hivyo kuwaweka katika hatari ya kunenepa kupindukia. Hii ni kwa mujibu wa watafiti kutoka Uingereza.

Chuo Kikuu cha Cambridge kiliwakusanya watu 54 kisha wakapewa mchuzi rojo wa kuku aliyekaangwa kwa mafuta. Pia wakapewa mchanganyiko wa matunda, ambayo hayakuwa matamu sana.Baadhi ya wale ambao jeni zao zinavutiwa na mafuta, waliula zaidi mchuzi rojo wa kuku kuliko matunda.

Haki miliki ya picha Thinkstock
Image caption Kuna watu ambao Jeni zao hazipendi matunda lakini chakula cha mafuta

Mtafiti mkuu Profesa Sadaf Farooqi kutoka taasisi ya utafiti ya ''Wellcome Trust Medical Research Council Institute of Metabolic Science'', kilichoko katika Chuo Kikuu cha Cambridge amesema utafiti wake umebainisha kwamba maumbile ya watu kwa kiwango fulani huwavutia kwa chakula fulani, na siyo kwa sababu ya uhuru wa kuamua.

Hata hivyo amesisitiza umuhimu wa lishe bora yenye maadini yote ya chakula na kufanya mazoezi ili kuwa na afya bora hususan uzani unaotakiwa.