Tshisekedi: Tutamuonyesha 'kadi nyekundu' rais Kabila

Kiongozi wa upinzani nchini DRC Etienne Tshisekedi
Image caption Kiongozi wa upinzani nchini DRC Etienne Tshisekedi

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ataonyeshwa kadi nyekundu iwapo atasalia mamlakani mnamo mwezi Disemba kulingana na kiongozi wa Upinzani Etienne Tshisekedi

Upinzani umehusika katika maandamano ya umma ukimtaka rais kabila kujiuzulu kwa sababu katiba inamzuia kusalia madarakani baada ya mwezi huo.

Hatahivyo ,maafisa wa uchaguzi wanasema kuwa uchaguzi unaotarajiwa mwezi Novemba utacheleweshwa kutokana na ugumu wa kuwasajili wapiga kura katika taifa la takriban watu milioni 30.

Akizungumza baada ya mkutano wa siku tatu wa muungano wa vyama vya upinzani katika mji mkuu wa kinshasa,Tshisekedi alisema kuwa tume ya uchaguzi inafaa kuvunjwa kwa kushindwa kuafikia mahitaji ya kikatiba ya kuitisha uchaguzi mwezi Novemba.

Takriban watu 17 waliuawa katika makabiliano na vikosi vya usalama mnamo tarehe 19 baada ya upinzani kufanya maandamano ya kutaka kusitishwa kwa utawala wa Kabila mnamo mwezi Disemba.

Tshisekedi alisema: Mnamo tarehe 19 mwezi Octoba,tutampatia kadi ya njano.Na iwapo hatakuwa amejiuzulu kufikia mwezi Disemba tutamuonyesha kadi nyekundu.