wapiganaji ''wawateka nyara'' watoto wachanga Nigeria

Wapiganaji nchini Nigeria
Image caption Wapiganaji nchini Nigeria

Maelezo yanaendelea kuzuka kuhusu kutekwa nyara kwa watu 11 wakiwemo watoto watatu wachanga katika kijiji kimoja cha mashambani kaskazini mwa jimbo la Nigeria la Bauchi,kulingana na mmoja wa watu wa familia hiyo IIlya Muhammad.

Wapiganaji waliteka watu hao kutoka katika kijiji cha Tipachi,takriban kilomita 120 kaskazini mwa mji mkuu wa jimbo hilo,mapema siku ya Jumatatu.

Bwana Muhammad aliniambia kwamba watekaji hao wanataka kulipwa fidia kupitia simu waliopiga.

Wanawake watatu,wasichana wanne na mvulana mmoja walitekwanyara pamoja na watoto watatu,aliongezea.

Watu watatu pia walijeruhiwa wakati wa uvamizi huo wa kijiji hicho,aliongezea Muhammad.

Mbunge mmoja wa jimbo hilo la Bauchi ,Abdullahi Sa'ad Abdulkadir alimuambia Muhammad kwamba polisi na wanajeshi wamepelekwa katika eneo hilo katika juhudi za kuwaokoa watu hao.

Kijiji hicho kiko katika eneo lenye msitu mkubwa ,na watu wengi wametekwa nyara katika siku za hivi karibuni.