App ya simu kupima saratani ya kizazi Tanzania
Huwezi kusikiliza tena

App ya simu kupima saratani ya kizazi Tanzania

Wakati saratani ya shingo ya kizazi inaweza kuzuiwa na hata kutibika ikigundulika mapema na kutibiwa kisahihi, ukosefu wa uchunguzi umechangia kutokea kwa vifo vingi sana.

Nchini Tanzania peke yake, takribani wanawake 4,000 wanafariki dunia kila mwaka kutokana na saratani hii, kwa mujibu wa shirika la afya duniani.

Katika kukabiliana na vifo hivi, watafiti wa masuala ya afya nchini Tanzania wametengenza programu tumizi- yaani APP inayoweza kusaidia upimaji wa saratani hii.

Mwandishi wetu Sammy Awami anatupasha zaidi kuhusiana na nyenzo hii.