Serikali ya Ghana kuiondoa sanamu ya Gandhi

Sanamu ya Mahatma Ghandhi
Image caption Sanamu ya Mahatma Ghandhi

Serikali ya Ghana imeitikia wito wa kuondolewa kwa sanamu ya Mahatma Gandhi kutoka katika ardhi ya chuo kikuu cha Ghana katika mji mkuu wa Accra,kulingana na AFP.

Ombi lililowasilishwa katika mitandao ya kijamii ambalo lilitiwa saini na zaidi ya watu 1,500 lilianzishwa na wasomi katika chuo hicho kikuu.

Walidai kwamba Gandhi ambaye amesifiwa na watu maarufu kwa kuisaidia India kupigania uhuru wake bila kumwaga damu kutoka kwa ukoloni wa Uingereza katikati ya karne ya 20 alikuwa na kitambulisho cha kibaguzi na alitoa matamshi ya kibaguzi dhidi ya Waafrika.

Chombo cha habari cha AFP sasa kinasema kuwa serikali inapanga kuipeleka mahala pengine sanamu hiyo.

Kimeinukuu taarifa ya waziri wa maswala ya kigeni aliyesema anataka kuhakikisha usalama wa sanamu hiyo na kuepuka tetesi zozote.