Kimbunga Hurricane Matthew chaua watu 100 Haiti

Miti iliyong'olewa na kimbunga hicho
Image caption Miti iliyong'olewa na kimbunga hicho

Siku mbili baada ya kuipiga nchi ya Haiti, kimbunga Hurricane Matthew kimeendelea kusababisha madhara makubwa hususan maeneo ya Kusini Magharibi mwa nchi hiyo.

Idadi ya watu waliokufa imefikia 100 wengi wakiwa ni kutoka mji wa Roche-à-Bateau na Jeremie.

Image caption Picha ya kbla na baada ya kimbunga hicho

Nyumba nyingi zimeharibika vibaya, huku wakaazi wake wakiachwa bila chakula na maji.

Mashirika ya kutoa misaada yanasema kuwa asilimia 80 katika baadhi ya maeneo zimehariwa vibaya, miti imengooka na mazao yamezolewa na maji.