Reli ya kwanza ya umeme Afrika yazinduliwa Ethiopia

Reli ya kwanza ya umeme Afrika yazinduliwa Ethiopia

Kwa mara ya kwanza Afrika imepata reli inayotumia umeme. Reli hiyo imezinduliwa nchini Ethiopia na itaunganisha mji mkuu wa Addis Ababa na mji wa pwani wa Djibouti.

Treni zitakuwa zikisafiri kwa kasi ya kilomita mia moja ishirini kwa saa - hivyo kupunguza muda wa usafiri mpaka chini ya nusu siku.

Viongozi wa nchi hizo mbili wamehudhuria uzinduzi wa mradi huo uliogharimu dola bilioni nne na kufadhiliwa China kwa kiasi kikubwa. Emmanuel Igunza anaripoti kutoka Addis Ababa.