Bango kubwa la Putin lawekwa New York

olisi walifika na kuliondoa muda mfupi baada ya picha za bango hilo kuanza kusambazwa sana katika mitandao ya kijamii. Haki miliki ya picha Reuters
Image caption olisi walifika na kuliondoa muda mfupi baada ya picha za bango hilo kuanza kusambazwa sana katika mitandao ya kijamii.

Bango kubwa lenye picha ya Rais wa Urusi Vladimir Putin, lililoandikwa "mweneza amani", limewekwa na watu wasiojulikana katika daraja la Manhattan jijini New York.

Bango hilo lililowekwa Alhamisi linamuonesha kiongozi huyo wa Urusi akiwa mbele ya bendera ya Urusi.

Daraja hilo maruufu huunganisha Manhattan na Brooklyn.

Polisi walifika na kuliondoa muda mfupi baada ya picha za bango hilo kuanza kusambazwa sana katika mitandao ya kijamii.

Kufikia sasa hakuna aliyekamatwa.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Polisi wanafanya uchunguzi

Uhusiano kati ya Washington na Moscow umedorora miezi ya karibuni.

Baadhi ya wanasiasa wameituhumu Urusi kwa kuingilia uchaguzi wa urais Marekani baada ya habari muhimu za chama cha Democratic kudukuliwa.

Mkataba wa kusitisha vita nchini Syria ambao ulikuwa umefanikishwa na nchi hizo mbili ulivunjika mwezi uliopita.

Marekani pia imesitisha mazungumzo ya kushirikiana na Urusi kushambulia wapiganaji wa Kiislamu.

Haki miliki ya picha Reuters

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii