Nyota Muislamu azuiwa kuigiza mchezo wa Kihindu India

Nyota wa filamu za Bollywood Nawazuddin Siddiqui Haki miliki ya picha Google
Image caption Nyota wa filamu za Bollywood Nawazuddin Siddiqui

Wahindi wa mrengo wa kulia wamemlazimisha nyota wa filamu za Bollywood Nawazuddin Siddiqui kutoshiriki katika hafla ya sherehe ya Kihindu,''kwa sababu ni Muislamu''.

Baadhi ya wanachama wa shirika la Kihindi la Shiv Sena walisema kuwa wanapinga muigizaji Muislamu mbele ya jukwaa huko Ramlila,ambapo sherehe za uigizaji zinazohusiana na dini ya Hindu Ramayana hufanyika mbali na taifa lote la India.

Nyota huyo alisema kuwa kushiriki katika sherehe hiyo ilikuwa ndoto yake tangu akiwa mdogo.

Shirika la Shiv Sena hutumia ghasia na vitisho ili kusukuma wazo ama ajenda yake.

Katika sherehe hiyo Wahindi husherehekea zuri dhidi ya ovu kufuatia ushindi wa mungu wa kihindi Ram dhidi ya shetani wa kifalme mwenye vichwa 10 Ravana .

Vijiji nchini India hufanya uigizaji huo na hutumia muda mwingi kujiandaa.