Tibaijuka:Kwa nini nilikataa fedha za tuzo nililoshinda
Huwezi kusikiliza tena

Tibaijuka: Kwa nini nilikataa fedha nilizopewa

Aliyekuwa mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi duniani UN habitat, Profesa Anna Tibaijuka hivi karibuni alikataa fedha takribani dola laki moja alizopewa baada ya kushinda tuzo ya Mfalme wa Bahrain Sheikh Khalid bin Ahmed Al Khalifa katika hali iliyozua maswali mengi kutokana na uamuzi wake huo.

Tuzo hiyo alipewa kwa mchango wake katika kuchangia maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa. mwandishi wetu Regina Mziwanda amezungumza na Profesa Anna Tibaijuka kutaka kujua kwanini alikataa fedha hizo.