Kijana aliyemea mkia afanyiwa upasuaji India

Kijana mwenye mkia nchini India afanyiwa upasuaji kuuondoa
Image caption Kijana mwenye mkia nchini India afanyiwa upasuaji kuuondoa

Kijana mwenye mkia wa sentimita 20 unaomea chini ya uti wa mgongo wake amefanyiwa upasuaji ili uondolewe

Ulianza kutokea katika mgongo wa kijana huyo wa miaka 18 baada ya siku yake ya kuzaliwa ya 14.

Yeye na familia yake kutoka Nagpur nchini India walifanya swala hilo kua siri kwa sababu walikuwa na wasiwasi angechokozwa na wenzake.

Sasa wanataka kuonana na daktari baada ya mkia huo kuendelea kumea mfupa ndani yake.

Mkia huo unadaiwa kuwa mrefu kuwahi kutokea kwa mwanadamu ijapokuwa visa kama hivyo ni vichache.

Image caption Mkia huo una urefu wa sentimita 20

''Ulianza kuwa tatizo baada ya kuanza kumea nje ya mwili wake'',alisema mamake ambaye hakutaka kutajwa jina.

''Angeinua mkia huo kila mara alipotaka kubadilisha nguo zake.Ningeona kwamba ilikuwa inakera na uchungu mkubwa kwake,kwa hivyo nilimpeleka hospitali''.

Madaktari wanasema kuwa kijana huyo huenda alimea mkia huo ndani ya tumbo la mamake kutokana na kasoro ya uti wa mgongo,lakini ukaonekana nje baada ya kijana huyo kuwa mkubwa.