Mkulima avumbua mashine ya kupanda ufuta Tz
Huwezi kusikiliza tena

Tanzania inaongoza barani Afrika na ya tatu duniani katika kuuza nje zao la ufuta

Tanzania inaongoza barani Afrika na ya tatu duniani katika kuuza nje zao la ufuta. Lakini ukulima duni wa jembe la mkono umekuwa ukiathiri sana biashara hii. Sasa mkulima Costantine Martin, ambaye yeye ameishia darasa la saba tu amevumbua mashine ya kupandia ufuta na tayari amenufaisha maelfu ya wakulima wenzake. Mwandishi wetu Sammy Awami alimtembelea kijijini kwake Babati mkoani Manyara, Kaskazini mwa Tanzania na kututumia ripoti hii