Yemen: Marekani yaionya Saudia kuhusu shambulio

Muungano unaoongozwa na Saudia ulishambulia mkutano wa mazishi Yemen
Image caption Muungano unaoongozwa na Saudia ulishambulia mkutano wa mazishi Yemen

Marekani imeionya Saudi Arabia dhidi ya shambulio la angani lililolenga sherehe moja ya mazishi nchini Yemen na kuwaua zaidi ya watu 140 na wengine wengi kujeruhiwa.

Inasema kuwa, mashambulio ya angani, yalioongozwa na majeshi ya muungano chini ya Saudi Arabia, katika mazishi hayo.

Mshirikishi mkuu wa Umoja wa mataifa nchini Yemen, Jamie McGold-rick, amesema kuwa wafanyikazi wa utoaji misaada, wameshtushwa mno na shambulio hilo, lililofanyika katika mji mkuu Sanaa.

Waombolezaji walikuwa wakitoa heshima zao za mwisho, kufuatia kifo cha babake kinara mmoja maarufu wa waasi.

Marekani inasema kuwa, inatathmini kupunguza uungaji wake mkono wa majeshi hayo ya muungano yanayoongozwa na Saudi Arabia.

Saudi Arabia, imekanusha kuwa ndege zake zilishambulia mkutano huo wa mazishi.